Pages

Pages - Menu

Wednesday, August 15, 2012

AT AFANYA NGOMA YA HIP HOP

WAKATI mwingine  unaweza usiamini lakini ukweli mfalme wa miduara Bongo Ramadhani Ally Tall 'AT' baada  ya kutamba sana  kwenye staili hiyo sasa ana ngoma ya Hip Hop ambayo ameigonga  nchini Sweden akimshirikisha  mtoto mmoja matata wa kibongo anayeishi huko ambayo ameipachika jina la ‘Tunafanya mambo’.
Ku-rap kwa msanii huyo ndani ya ngoma hiyo kumekuja baada ya mtoto huyo kutaka kufanya kazi ya pamoja lakini awe ana Rap, hivyo anaamini watu watamuona tofauti kidogo ingawa kwa upande wake anaona muziki wowote anaweza kufanya huku akiahidi kuwa  video ya ngoma hiyo inaanza kupigwa picha kesho ili kuipa nafasi ya kuitoa pamoja na  audio.

“Uwezi amini nimefanya ngoma ya Kurap na najua watu watu watanichukulia tofauti sana lakini najua uwezo wangu ni mkubwa katika kila aina ya muziki ninaotaka kufanya,…
WAKATI mwingine  unaweza usiamini lakini ukweli mfalme wa miduara Bongo Ramadhani Ally Tall 'AT' baada  ya kutamba sana  kwenye staili hiyo sasa ana ngoma ya Hip Hop ambayo ameigonga  nchini Sweden akimshirikisha  mtoto mmoja matata wa kibongo anayeishi huko ambayo ameipachika jina la ‘Tunafanya mambo’.
Ku-rap kwa msanii huyo ndani ya ngoma hiyo kumekuja baada ya mtoto huyo kutaka kufanya kazi ya pamoja lakini awe ana Rap, hivyo anaamini watu watamuona tofauti kidogo ingawa kwa upande wake anaona muziki wowote anaweza kufanya huku akiahidi kuwa  video ya ngoma hiyo inaanza kupigwa picha kesho ili kuipa nafasi ya kuitoa pamoja na  audio.
“Uwezi amini nimefanya ngoma ya Kurap na najua watu watu watanichukulia tofauti sana lakini najua uwezo wangu ni mkubwa katika kila aina ya muziki ninaotaka kufanya, na hii kazi itakuwa na uwezo wa kusikilizwa popote pale kutokana na uzuri wake,” alisema.
Hata hivyo aliongeza kuwa baada ya ngoma hiyo atakuwa katika maandalizi yake mengine ya kutoa kazi mpya, ambayo bado hajajua ipi itakayokwenda hewani kwani amefanya kazi mbili na wasanii mahiri wa taarabu moja na Hadija Kopa na nyingine na Mzee Yusuph.
“Kuna ngoma mbili ambazo sijajua ipi itaanza kwenda hewani hivyo nahitaji kukaa na wadau ili waweze kunishauri niitangulize ipi ingawa ngoma zote ni kali sana,” alisema.

No comments:

Post a Comment