Rita Paulsen ‘Madam Rita’.
CHIEF
Judge wa Shindano la Epiq Bongo Star Search, Rita Paulsen ‘Madam Rita’
hivi karibuni amejikuta akiombwa uchumba na vivulana nyenye umri mdogo
‘serengeti boys’ kupitia ukurasa wake wa Facebook.
Akipiga stori na Mwandishi wetu , Madam Rita alisema kuwa, alianzisha
ukurasa huo kwa ajili ya kubadilishana mawazo na watu mbalimbali lakini
akashangazwa na baadhi ya wavulana ambao wamempenda kiasi cha kufikia
hatua ya kumuomba uchumba.
“Huwezi amini sina siku nyingi sana tangu
nimeanzisha ukurasa huu lakini nina marafiki wengi na wapo ambao
wanaomba kuwa marafiki wangu, huko nimeshapata wachumba sita tena
wengine wakiwa na umri mdogo sana,” alisema Madam Rita na kuongeza:
“Kimsingi nawaheshimu watu wa rika zote kutoka
mikoa yote kwani wao ndiyo wadau wakubwa wa EBSS na wameifanya program
hii kujipatia umaarufu mkubwa na kufika hapa ilipo sasa.”
MADAMU RITA AOMBWA UCHUMBA NA ‘SERENGETI BOY’

No comments