Pages

Pages - Menu

Friday, August 10, 2012

''SHETA KUWAPA SHAVU UNDERGROUND''

     Msanii anayetamba na wimbo wa nidanganyedanganye aliomshirikisha diamond platnumz Shettah a.k.a king Mswatti au Baba kijacho amefunguka juu ya kuanzisha lebo yake ya muziki ili kuendeleza na kukuza muziki wa kizazi kipya maarufu kama Bongo flavour
     Akiongea juu ya swala hilo Shetta amesema kuwa Lebo hiyo itakuwa na wasanii wenye vipaji ili kuleta ushindani katika gemu ya kizazi kipya na hatimaye kuinua mziki wa Bongo flavour
     Kwa sasa shetta ameanza kupokea Demo za wasanii mbalimbali ili kuziangalia na kufanya uchaguzi wake wa nani achukuliwe na nani asichukuliwe kwenye lebo yake hiyo
     Kama wewe msanii na upo Mkoani unajijua una kipaji huu ndio muda wako kwani sheta amesema kwamba unawezakutuma demo yako kwa shettamusic@gmail.com demo yako itamfikia mara moja.......!!! na unaweza kuchaguliwa kuingia kwenye lebo hiyo

No comments:

Post a Comment