Random Posts

Powered by Blogger.

Contact us

www.mau2ndudj.blogsport.com

email--mau2ndudj@gmail.com
-philymonjohn@yahoo.com
-josephm39bongo@yahoo.com

simu -
-0764277248
-0719184760

Special offer

Mau2ndu djz @Copyright 2012

Ads 468x60px

Social Icons

Featured Posts

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

MAU2NDU DZJ KWENYE FULL SWAGZZ NA MASTORY KIBAO

Lorem 1

Technology

Circle Gallery

Shooting

Racing

News

Lorem 4

» »Unlabelled » ''ALIYEKUWA RAIS WA SHIRIKISHO WA NGUMI ZA RIDHAA TANZANIA {BFT} SHAABAN BINTANGA AACHIWA HURU''

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imeamua kufunga ushahidi wa upande wa Jamhuri katika kesi inayomkabili Rais wa zamani wa Shirikisho la Ngumi za Radhaa Tanzania (BFT), Alhaji Shaaban Mintanga, baada ya kushindwa kuleta mashahidi watano kutoka nchini Mauritius kwa muda mrefu. Mintanga ameachiwa huru baada ya kusota rumande tangu
April 4 mwaka 2008. Uamuzi huo umetolewa leo na Jaji Dk. Fauz Twaib anayesikiliza kesi hiyo, baada ya kukubaliana na ombi la jopo la mawakili waomtetea Alhaji Mintanga la kuiomba kufanya hivyo kwa mamlaka iliyokuwa nayo kwa mujibu wa sheria. Alhaji Mintanga leo aliwakilishwa na mawakili Berious Nyasebwa, Aliko Mwamanenge na Jerome Msemwa huku upande wa Jamhuri ukiwakilishwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Prosper Mwangamila na Wakili wa Serikali, Hamidu Mwanga. Akitoa uamuzi huo, Jaji Dk. Twaib alisema kwa muda wa vipindi vinne vya mahakama, upande wa Jamhuri umeshindwa kuleta mashahidi na kila mara umekuwa ukitoa hoja za kuomba kuahirishwa, ukosefu wa fedha, unafanya mawasiliano na kutumwa ofisa Mauritius na pia kwa vipindi hivyo umekuwa ukileta mawakili tofauti. Jaji Dk. Twaib aliahirisha shauri hilo hadi Septemba 7, mwaka huu, ambapo upande wa Jamhuri na wa utetezi utawasilisha hoja hizo kabla ya mahakama kutoa uamuzi iwapo inaona Alhaji Mintanga ana kesi ya kujibu au la.
Mintanga anakabiliwa na mashitaka mawili ya kula njama na kusafirisha dawa za kulevya zenye uzito wa kilo 4.8 kutoka nchini Tanzania kwenda nchini Mauritius. Dawa hizo zinadaiwa kuwa na thamani ya sh. milioni 120.

About MAU2NDU DJ'S

WePress Theme is officially developed by Templatezy Team. We published High quality Blogger Templates with Awesome Design for blogspot lovers.The very first Blogger Templates Company where you will find Responsive Design Templates.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

Leave a Reply