Msanii wa THT Lameck Ditto ameshindwa kutamba kwenye tuzo za the RFI
France 24 Discoveries Awards 2012 alizokuwa ametajwa kuwania. Mwanamuziki wa
nchini Namibia Elemotho Gaalelekwe ndiye aliyeibuka mshindi. Wasanii wengine
waliokuwa wakiwania tuzo hizo ni
pamoja na Maryse Ngalula (DRC), Spyrow (Cote
d’Ivoire), Denis Larose (Mauritius), GT the Guitarman (Nigeria), Tafeifa
(Senegal), Nasser (Mauritania) na Trio Teriba (Benin). Mshindi huyo atazawadiwa
kiticha cha €10 000, kupewa promotion, kutumbuiza kwenye tamasha kubwa mjini
Paris Ufaransa na ziara barani Afrika.
No comments:
Post a Comment