Mkali wa miondoko ya crunk bongo C pwaa leo ameongea kupitia Powerjams ya East Africa Radio baada ya kutoka Afrika ya Kusini kuwa pamoja na kwamba hakurudi na Tuzo lakini amegundua kwamba muziki wake umefika mbali kuliko alivyokuwa anadhani.Cpwaa anasema kuwa tangu afike alikuwa akitafutwa afanye mahojiano na vituo mbalimbali vya redio, "lakini kikubwa ni kwamba nimerudi na habari nzuri kuwa niko na mipango ya kufanya kazi na
msanii mkubwa wa Ghana D-Black, msanii mwingine wa Afrika ya Kusini na pia Navio kutoka Uganda", Cpwaa.Msanii huyo pia alizungumzia kuhusu ngoma mbili hivi karibuni 'Mambo' na 'Mission 12 0'Clock' kuwa video zake zinakuja na kama kawaida zitakuwa kali ili kuweza kufikisha muziki wetu kimataifa.
No comments:
Post a Comment