KUTOKANA na malalamiko ya baadhi ya mashabiki na hali ya kutofahamu juu
ya sababu inayosababisha kuendelea kuonyeshwa kwa tangazo la kampuni ya
simu ya mkononi Airtel lilikouwa limerekodiwa na marehemu
Sharomilionea, King Majuto afafanua sababu zinazosababisha tangazo hilo
kuendelea kuwa hewani kwa kipindi hiki
Akizungumza kwa njia ya simu Amri Athumani a.k.a King Majuto alisema
kuwa mkataba bado unaendelea kuwepo na ndio maana bado tangazo hilo
linaendelea kuchezwa katika vyombo vya habari
Alisema kuwa mbali na mkataba huo pia mama yake mzazi na marehemu
Sharomilionea ameomba tangazo hilo liendelee kupigwa ili kwa kipindi cha
mwezi mmoja ili aweze kupata fedha za kujikimu kimaisha kwa kipindi
hiki ambacho mwanaye ndiye alikuwa msaada mkubwa kwake
"Tangazo hilo linapigwa kwa makubaliano ya mama yake mzazi ili aweze
kupata fedha za kujikwimu , na ameruhusu lipigwe kwa kipindi cha mwezi
mmoja na ndio maana unaona linachezwa hilo tangazo katika vyombo vya
habari" alisema King Majuto
Mbali na hayo alipouulizwa mwanasheria wa kujitegemea Mwemezi Makumba
juu ya uhalali wa kuendelea kulicheza tangazo hilo yeye alieleza
kuwa,kama taratibu zote zilifuatwa na kukamilika katika mkataba huo ni
halali kuendelea kucheza tangazo hilo huku mafao pamoja na stahiki zote
za marehemu zikilipwa kwa mrithi wake
Alisema kuwa kulingana na taratibu za mkataba kukamilika mtu anapokufa
na mkataba haufi, bali unaendelea kwa kushirikisha warithi wa marehemu
Aliongezea kuwa mkataba unaweza kufa kama taratibu za mkataba huyo haujakamilika kisheria
No comments:
Post a Comment