Nyimbo zimepata umaarufu kupitia waimbaji wake na si ubunifu uliopo ndani ya kazi, huku vipaji vipya kila siku vimeonekana kujitokeza
Akielezea tasmini hiyo msanii mkongwe wa muziki wa bendi John Kitime alisema kuwa muziki umekuwa kwa asilimia kubwa ukitofautisha na kipindi cha nyuma huku waimbaji wakionekana kuongezeka siku hadi siku hali hiyo inaleta changamoto kubwa katika sekta ya muziki hususani wa kizazi kipya ambapo huko kumeonekana kuzaliwa kwa vipaji vipya kila siku
Alisema kukua kwa muziki huo kumesababishwa na nyimbo kupata umaarufu kupitia waimbaji wake, kitendo hiko kimesababisha kutopata nyimbo bora kutokana na chombo cha muziki
Alisema kuwa kwa upande wa bendi mwaka huu kumeonekana Waimbaji kupata umaarufu na kuchukuliwa kwenye bendi nyingine kwa dau kubwa huku wapigaji kuonekana bado wapo na kazi zao kutopata thamani wala kutambulika kwa jamii
Kitime alisema kwa mwaka 2013 anategemea kuwa na mabadiliko makubwa kwenye sekta ya muziki kiujumla hususani kwenye upande wa upigaji vyombo ambapo huko watatumia vizuri vyombo hivyo na kuleta ubunifu mkubwa ili kazi itambulike na kuthaminika duniani kote
Alisema kuwa kwa upande wa muziki wa bendi anatarajia watakuja na kitu cha tofauti na kuacha kuiga mawazo na ubunifi wa wanamuziki kutoka nchini Kongo, na kuanza kuamini cha kwao na kuwa wabunifu ili kuweza kuboresha kazi yao pamoja na kuleta utofauti
Kitime alizungumzia upande wa muziki wa kizazi kipya alisema kuwa kwa mwaka huu anatarajia kuona mabadiliko makubwa na wasanii kuacha kuiga tamaduni za nje na kutumia katika nyimbo zetu
Alitoa wito kwa wasanii kuwa na mawazo ya kutumia cha kwao kwa kuwa wabunifu na kuendeleza 'idea' ya midundo ya kizaramo ambayo teyari wameshaanza kuitumia katika nyimbo ili waweze kutambulika kwa aina hiyo
"Nyimbo zetu haziwezi kuvuka mipaka kama hatakuwa teyari kubadilika kwa kuongeza ubunifu na kuacha kabisa kucop nyimbo za watu kwani ukisikiliza baadhi ya nyimbo za sasa nyingi zimejaa miondoko ya kwaito ambayo siyo ya kwetu ni ya South Afrika kwa hiyo hauwezi kuvuka katika mipaka ya kimataifa na idea za watu lazima tuwe na cha kwetu" alisema Kitime
No comments