
BAADHI ya wasanii wa filamu nchini Tanzania watoa maoni yao juu ya utangazaji wa kazi zao kwa ngazi ya kimataifa itakayofanywa na kampuni ya Mad Mad iliyopo nchini London Uingereza
Mmoja wa wasanii hao ambao wametoa maoni yao ni pamoja na Steven Nyerere alisema anaamini kampuni hiyo itafanya kazi vizuri na wasanii huku wakiwa wanannafasi kubwa ya kutangaza kazi zao kimataifa
Alisema wasanii wanatakiwa kujiandaa kimataifa huku wakitoa ushirikiano wa kutosha kwenye kampuni hiyo yenye lengo la kuinua kipato cha wasanii wa filamu nchini
Steven aliweka wazi kuwa watatoa kipaumbele kwenye matumizi ya lugha ya kiswahili hivyo watatumia lugha hiyo kwa asilimia kubwa ili kutangaza lugha hiyo kimataifa
Alisema kuwa teyari wameshaanza maandalizi ya kutengeneza filamu ambayo itakayoingizwa katika soko la kimataifa inayokwenda kwa jina la Kongo akiwa ameshilikishwa msanii maarufu wa nyimbo za Kikongo Fally Ipupa pamoja na nyota wa hapa bongo akiwemo Dk. Cheni na wengineo
"Katika filamu hiyo itatumika lugha pia ya kiswahili ili kujitangaza na kutangaza kazi zao , filamu ambayo itatumia muda mrefu kutengeneza ili itoke kwenye ubora mzuri tofauti na filamu zinazotengenezwa wiki mbili" alisema Nyerere
Wakati huo huo baadhi ya wasanii wengine wanaonekana kutokupata taarifa kwa wakati kuhusu kazi ya kampuni hiyo hali hiyo inaonyesha wasiwasi wa utendaji kwa upande wao wa kisanii
Monalisa ambaye pia ni msanii mkongwe yeye alisema kuwa kampuni haijui na hajawahi kuhisikia hivyo anashindwa kuongelea chochote wala kutoa mawazo yoyote ya nini kifanyike ili kuboresha kazi zao
Akiongelea kuhusu ukuzaji wa kipato cha wasanii kutokana na kutangaza kazi zao kimataifa alisema hanauwakika kuhusu hilo kwani kunakuwa na matatizo kwa waongozaji wa filamu kuwalipa wasanii bila ya kujua thamani ya pesa inayotoka na inayoingia
Pamoja na hayo Monalisa alishangazwa na kitendo cha baadhi ya wasanii kuwa wabinafsi kwa kuto toa ushirikiano wa kutosha ili kuboresha kazi zao za sanaa
No comments:
Post a Comment