HAYA NDIO MAMBO KUMI USIYOYAJUA KUHUSU MSANII GYAN BOBIC KUTOKA KUNDI LA THE SWITCH.
1.Jina lake halisi ni Gyan Feymon.
2.Bobic ni jina lililotokana na kuwa na uwezo mkubwa wa kusakata kabumbu hivyo kupelekea wenzake kumfananisha na mchezaji wa zamani wa ujerumani Fredy Bobic.
3.Bobic alizaliwa katika hospitali ya Meta iliyopo jijini Mbeya ze green city wakati kabila lake ni
Mnyakyusa.
4.Bobic ni member wa ‘’The switch’’ kundi lililo ndani ya wakacha likiundwa na Gyan Bobic mwenyewe,Josh joh na Abba moko.
5.Kwa sasa ni mwanachuo katika chuo kikuu cha Tumaini akisomea digree ya biashara.
6.wakati Bobic alipokuwa mdogo alikuwa akimiliki daftari kama saba hivi zikiwa na mashairi na hiki ni kiashirio tosha kuwa kijana huyu alianza kuupenda muziki toka way back.
7.Tayari ameshafanya kazi na Prodyuza Mesen Selekta katika nyimbo zake ambazo ni Nikubali ambayo aliwashirikisha Steve rnb na Izzo Bizness na nyingine inayoitwa niambie Mesen akiimba chorus.
8.Kwa sasa anatamba na ngoma yake inayoitwa My everything iliyotengenezwa katika studio za pyrex records chini ya Prodyuza Erick tup.
9.Mtu aliyemvutia kuingia kwenye sanaa ya muziki ni Fanani aliyekuwa member wa kundi la hardblasters kundi lililokuwa likiundwa na Profesa Jay,Big will na mwenyewe Fanani.
10.Bobic na wenzake wanaounda kundi la ‘’the switch’’ wanaproject nyingi ikiwa ni pamoja na kutoa tshirt kama #team de switch,shine 2 infinity na my status ndo event zao tshirt zilizofanya poa sana sokoni.
No comments