Suma
Mnazaleti na aliyekuwa meneja wa Mtanashati Entertainent, Maneno
wamefukuzwa Mtanashati Entertainment kutokana na kuonesha utovu wa
nidhamu.
Akiongea na mau2ndu kwenye jana , mkurugenzi
wa kampuni hiyo Ustaadh Juma amesema meneja huyo amekuwa akitumia cheo
chake vibaya na pia kuwa na tabia ya kutoa siri za kampuni.
Amesema zaidi ni jana
kwenye fainali za kipindi cha Bibi Bomba baada ya meneja huyo
kushindwa kufanya kazi yake inavyotakiwa ya kuwaangalia wasanii wake
ambao jana walilewa kiasi cha kuiabisha kampuni yake.
Amesema Suma
Mnazaleti amekuwa na tabia chafu kiasi cha kuwaharibu wasanii wake
ambapo PNC alikuwa ameacha kunywa pombe lakini tangu Suma ajiunge nao,
PNC amerudia kunywa pombe.
Hata
hivyo Meneja Maneno ambaye naye amehojiwa amedai kuwa yeye ndiye
ameacha kazi baada ya kuona ubabaishaji mwingi kwenye kampuni hiyo.
"Baada
ya party ya Bibi Bomba, wasanii wote wametembea kwa mguu wengine mpaka
Mwenge, yeye keshachomoka, alichokifanya ni kumchukilia tu Taxi Dogo
Janja, halafu leo hii unaondoka unasema wewe ni mtanashati," alisema.
"Meneja
huna hata shilingi kumi, unabeep unafanya nini, kwanini nisifanye kazi
zangu binafsi. Mimi ndo nimekataa na nimeikataa hiyo Mtanashati lakini
naweza nikakuonesha meseji , mimi ndo nimemwambia sitaki sio kwamba
yeye ndio kanitumia, hana uwezo wa kunitumia yule mimi."
No comments