Pages

Pages - Menu

Tuesday, September 25, 2012

''BAADA YA KUZINGULIWA NA PSQUARE MR MAY D AANZISHA LEBO YAKE YA MUZIKI''

     Ikiwa ni siku chache tangu aondolewe katika lebo ya ''square records'' inayomilikiwa na waliokuwa  maswahiba zake Peter and Paul{P SQUARE} msanii aliyefunika katika nyimbo ya
chop my money ya p square, Mr May d ameamua kuanzisha lebo yake ya muziki.

   Msanii huyo kutoka nigeria amesema kuwa lebo hiyo inayoitwa ''Confam Entertainment'' ni lebo ambayo atakuwa inahusika na muziki tofauti tofauti akidokeza kuwa atahusika sana na wanamuziki kutoka united kingdom{UK}.
    Kutokana na mr May d kuanzisha lebo hiyo inasemekana ni kuleta ushindani na pquare kwani toka msanii huyo aondolewe kienyeji square records amekuwa akitafuta njia ya kujitangaza kivyake.
    Kabla ya kusaini mkataba na p square katika lebo yao ya  square records mr may d alikuwa akifanya kazi zake katika lebo ya ''ice cream records''.

No comments:

Post a Comment