Leo tarehe 29 mwezi wa tisa mwaka 2012 ni siku ya kuzaliwa ya member wa kunndi la wateule anayejulikana kwa jina la Jaffarai au Jaffarymes.
Katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa mteule huyo ameamua kuzindua ofisi yake inayojishughulisha na kuosha magari maarufu kama
''car wash''.
Jaffarai amefunguka kuwa ameamua kufanya biashara hiyo ya kuosha magari kwasababu ameona kuna uhaba mkubwa wa car wash kwani muda tofauti amekuwa akikutana na foleni kubwa pale anapoenda kuosha gari yake katika car wash tofautitofauti hapa jijini.
Ofisi hiyo ya Jaffarai ipo mikocheni oil com karibu na TMJ hospital
''HONGERA JAFFARAI KWA SIKU YAKO YA KUZALIWA NA MAFANIKIO''
No comments:
Post a Comment