Pages

Pages - Menu

Tuesday, September 4, 2012

WEMA SEPETU AMWAGA MACHOZI JUKWAANI BAADA YA KUAMBIWA KUWA YEYE NI KICHECHE KAMA BONGO FLEVA


JINAMIZI linazidi kuwaandama wasanii  wa tasnia ya filamu  baada  ya  mwanadada mwenye mikasa kutoka Bongo movie Wema Sepetu kumwaga chozi back stage wakati mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya yaani Bongo fleva Emmanuel Elibariki Ney wa Mitego’ alipopanda Jukwaani na kusema Bongo fleva ni kicheche kama Wema Sepetu.


Vincent Kigosi, Wema Sepetu, Jacob Stephen, Aunty Ezekiel, Setven Mangere
 Wasanii wa Bongo movie wakisakata muziki katika uwanja wa CCM Kirumba

Chanzo chetu cha habari kimesema kuwa Ney alipopanda Jukwaani na kuchana freestyre na kulinganisha Bongofleva kicheche kama Wema Sepetu umati uliokuwa uwanjani ulilipuka kwa furaha na kumshangilia Ney akiwa sambamba na Dallaz Ukuni mwanamuziki mwenzake.

Kufuatia hali hiyo Jacob Stephen ‘JB’, Aunt Ezekiel wakiwa na Steven Nyerere walizua zogo lilotengeneza fujo wakitaka kumvamia Ney na kumpiga huku JB akilalama kwa kusema kuwa Ney amekuwa akiwadhalilisha kwa kutumia nyimbo zake.

Wakati hayo  yakifanyika Vincent Kigosi ‘Ray the Greatest’ alionyesha busara zake kwa kutoshiriki ugomvi huo.

Emmanuel Elibariki


 Msanii wa muziki wa Bongofleva aliyemliza Wema Sepetu kwa kuufananisha muziki wa Bongo fleva kicheche kama Wema Sepetu.

Aunty Ezekiel Wema Sepetu 
    Aunty Ezekiel akisakata Rumba na Wema Sepetu.

Aunty Ezekiel Wema Sepetu
   Aunty Ezekiel na Wema wakiwa wamejiachia
“Sasa hawa mbona wanataka kutuharibia show yetu vipi? Kwanza huyu aliyeitwa kicheche hata hajamaindi lakini wapambe ndio nawaona wanataka kulianzisha mbona mwenzao Ray katulia?" alihoji Samson Masanja mkazi wa Mwanza.

No comments:

Post a Comment