MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imeamua kufunga ushahidi wa upande wa Jamhuri katika kesi inayomkabili Rais wa zamani wa Shirikisho la Ngumi za Radhaa Tanzania (BFT), Alhaji Shaaban Mintanga, baada ya kushindwa kuleta mashahidi watano kutoka nchini Mauritius kwa muda mrefu. Mintanga ameachiwa huru baada ya kusota rumande tangu
April 4 mwaka 2008.
Uamuzi huo umetolewa leo na Jaji Dk. Fauz Twaib anayesikiliza kesi hiyo, baada ya kukubaliana na ombi la jopo la mawakili waomtetea Alhaji Mintanga la kuiomba kufanya hivyo kwa mamlaka iliyokuwa nayo kwa mujibu wa sheria.
Alhaji Mintanga leo aliwakilishwa na mawakili Berious Nyasebwa, Aliko Mwamanenge na Jerome Msemwa huku upande wa Jamhuri ukiwakilishwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Prosper Mwangamila na Wakili wa Serikali, Hamidu Mwanga.
Akitoa uamuzi huo, Jaji Dk. Twaib alisema kwa muda wa vipindi vinne vya mahakama, upande wa Jamhuri umeshindwa kuleta mashahidi na kila mara umekuwa ukitoa hoja za kuomba kuahirishwa, ukosefu wa fedha, unafanya mawasiliano na kutumwa ofisa Mauritius na pia kwa vipindi hivyo umekuwa ukileta mawakili tofauti.
Jaji
Dk. Twaib aliahirisha shauri hilo hadi Septemba 7, mwaka huu, ambapo
upande wa Jamhuri na wa utetezi utawasilisha hoja hizo kabla ya mahakama
kutoa uamuzi iwapo inaona Alhaji Mintanga ana kesi ya kujibu au la.
Mintanga
anakabiliwa na mashitaka mawili ya kula njama na kusafirisha dawa za
kulevya zenye uzito wa kilo 4.8 kutoka nchini Tanzania kwenda nchini
Mauritius. Dawa hizo zinadaiwa kuwa na thamani ya sh. milioni 120.
No comments:
Post a Comment