Leo tarehe 14 mwezi wa kumi tunatimiza miaka 13 tangu hayati mwl. Julius Kambarage Nyerere kututoka duniani na kutuacha wenye majonzi tele mioyoni mwetu.
Kamwe mtu huyu hatakuja kusahaulika kwani ni mtu wa kipekee kutokana na namna alivyokuwa kiakili na uongozi pia.Sidhani kama kwa tanzania ya sasa kutakuja kutokea kwa kiongozi kama huyu ambaye ataweza kuiongoza nchini kama hayati Baba wa taifa.
Viongozi wengi wa sasa wamekuwa na tamaa ya kujilimbikizia mali na
kujali familia zao kwa kuchukua fedha za wanachi ambazo ni pato linalotokana na kodi za wanachi.
Tumekuwa tukishuhudia siku hizi kwa kiongozi kuwa na mali nyingi za dhamani mfano tumeona baadhi ya viongozi wakinunua nyumba zenye dhamani ya fedha kama sh........................... sidhani kwa kiongozi mwenye maadili kama ni sahihi kwa mtu kumiliki mali hizi huku ukweli ukionesha kuwa ni dhahiri viongozi wetu ni mafisadi.
KWA UFUPI HUYU NDIYE HAYATI MWL. NYERERE ''HAPA CHINI''
Hayati mwl Julius Nyerere alizaliwa katika kijiji cha butiama tarehe 13 mwezi wa 4 mwaka 1922 mwl Nyerere ndie mtu aliyeisaidia nchi ya Tanzania kupata uhuru.Alikufa tarehe 14 octerber 1999 huko London Uingereza.
Alisoma Makerere University {1943-1945} na baadae kusoma University of Edinburgh {1949-1952}.Hayati mwalimu Nyerere alikuwa na watoto 7 ambae ni Rosemary Nyerere,Anna Nyrere,Magige Nyerere,Andrew Nyerere,Madaraka Nyerere,John Nyerere na Makongoro Nyerere.
''Pia amewahi kupata tuzo ya Jawaharld Nehru Award''
No comments:
Post a Comment