Tanzania inajipanga kuchukua hatua kama waliochukua wakenya kwa kuzizima simu zote ambazo si original maarufu kama simu za kichina au
simu bandia.
Kauli hii imetolewa na kaimu meneja mawasiliano wa mamlaka ya mawasiliano nchini {TCRA}Bw Semu Mwakyanjala ambae amesema kuwa mamlaka hiyo itaanza kwa kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kununua na kutumia simu halali.
Semu Mwakyanjala ameliambia gazeti la daily news jumapili kuwa hatua hiyo itachukuliwa na nchi zote nchi wanachama wa jumuiya ya afrika mashariki ikihusisha Burundi,Rwanda, na Uganda wakati Kenya tayari wamezizima simu hizo.
Lakini pia jambo hili limeonekana kutopokelewa vizuri na makampuni ya simu hapa nchini kwani wamepokea kwa shingo upande kwa kudhani kuwa watapoteza wateja wengi.
Kwa upande wa ndugu zetu wa Uganda mamlaka ya mawasiliano nchini humo {UCC} imesema kuwa itafanya tukio hilo la kuzima simu feki mwezi novemba mwaka huu.
''KAZI KWETU SISI TUNAOTUMIA SIMU FEKI''
No comments:
Post a Comment