Ikiwa ni siku chache tuu taifa la Nigeria limetoka kuingia katika majonzi ya kumpoteza mwanamuziki Goldie Harvey,tasnia ya maigizo nchini humo imeendelea kuwapota nguli wa filamu baada ya jana kumpoteza nguli mwingine aliyekuwa anajulikana kama Justus Esiri.
Justus Esiri aliyefariki akiwa na miaka 71 amewahi kutamba na muvi nyingi zilizo mpatia umaarufu kama ''Behind me'' na nyinginezo nyingi.
Marehemu ameacha mke na watoto sita huku miezi michache iliyopita mwanamuziki kutoka nchini Nigeria Dr sid aliuambia umma kuwa justus esiri ni baba yake mzazi kwa yeye jina lake halisi ni Onoriode Esiri.
Mwaka uliopita tasnia ya filamu nchini Nigeria iliwapoteza waigizaji nguli wawili ambao nao pia kama kwa Justus walikuwa ni wazee,Marehemu Peter Eneh alikufa november 25 mwaka jana wakati Enebeli Elebuwa alifariki december 4 mwaka jana huko new delhi india.......
''RIP JUSTUS ESIRI''
No comments:
Post a Comment