Lil’ Wayne ambaye amekuwa akitumiwa kwenye matangazo ya Mountain Dew
tangu mwaka 2012, ameikasirisha familia ya Emmitt Till kwenye wimbo
“Karate Chop” ambapo Weezy anasikika akisema, “Pop a lot of pain pills,
’bout to put rims on my skateboard wheels … beat that p***y up like
Emmett Till.”
Emmett Louis Till alikuwa ni mmarekani mwenye asili ya Afrika aliyeuawa
huko Mississippi mwaka 1955 akiwa na miaka 14 baada ya kumtongoza
msichana wa kizungu.
Licha ya kutuma barua ya kuomba radhi kwenye familia hiyo, ilikataliwa na ndugu zake pamoja umma kumkosoa vikali Lil Wayne.
Japo kampuni ya Pepsi haijatoa maelezo zaidi, hatua hiyo ilitangazwa na
msemaji wa Lil Wayne Sarah Cunningham, aliyesema kuwa ni kutokana na
kupishana kiubunifu.
YALIYOMPATA RICK ROSS, SASA YAMPATA LIL WAYNE. MKATABA WAKE NA MOUNTAIN DEW WAPIGWA CHINI

No comments