HATIMAYE
kile kitendawili cha muda mrefu cha Nani ata twaa taji la Redds Miss
Tanzania 2012, kimeteguliwa usiku wa Novemba 3, 2012, baada ya Mrembo
kutoka Kitongoji cha Sinza na Kanda ya Kinondoni jijini Dar es Salaam,
Brigitte Alfred kutwaa taji hilo.
Brigitte
ambaye nyota yake katika mashindano hayo ya urembo nchini ilianza
kung’aa tangu Kitongoji cha Sinza baada ya
kutwaa taji la Sinza na Baade kutwaa Taji la Redds Miss Kinondoni amedhihirisha ukali wake baada ya kuwabwaga warembo wenzake 29 waliokuwa wakiwania taji hilo kutoka Kanda mbambali.
kutwaa taji la Sinza na Baade kutwaa Taji la Redds Miss Kinondoni amedhihirisha ukali wake baada ya kuwabwaga warembo wenzake 29 waliokuwa wakiwania taji hilo kutoka Kanda mbambali.
Mpinzani
mkubwa wa Brigitte katika shindano hilo alikuwa ni Mrembo kutoka Kanda
ya Ziwa ambaye nae alianza kuwika baada ya kutwaa taji la Redds Mkoa wa
Mara na baade kutwaa taji la Kanda ya Ziwa, Eugene Fabian.
Enagene
alifanikiwa kushika nafasi ya pili katika shindano hilo kubwa ambalo
Brigitte ameondoka akiendesha gari aina ya NOAH na kitita cha Shilingi
Milioni 8.
Nafasi
ya tatu ilikwende kwa Malkia wa Kitongoji cha Kigamboni City na Miss
Temeke 2012, Edda Sylvesta huku nafasi ya Nne ikichukuliwa na Mrembo wa
Dar Indian Ocean na Kinondoni, Magdalena Roy na nafasi ya Tano ikienda
Kanda ya Ziwa tena kwa Mkoa wa Mwanza, Happyness Daniel.
No comments