Ustadhi Juma na musoma akiwa na Dj choka |
![]() | |||||||||||||||||||||||||||
Mmoja kati ya Xmember wa kundi la Mtanashati Entertainment Suma mnazareti |
Maneno amesema kuwa jana ustadhi juma na musoma alifika nyumbani kwa maneno na kumkuta mke wa maneno na kumtolea maneno ya vitisho huku akiwa na Dogo janja na mtu aliyekuwa kavaa nguo nyeusi zote kitu kilichomfanya mke wa maneno kutomtambua vizuri.
Baada ya ustadhi juma na musoma kufika kwa maneno na kumkosa alimwambia mke wa maneno kuwa maneno anatafutwa na polisi na baadae kidogo ndipo ustadhi juma na musoma alipoanza kutuma massage za vitisho kwa maneno zikimwambia kuwa yeye ni mtu mdogo sana hapa mjini kwa hiyo atampoteza!!! Kwa sasa Maneno amesharipoti katika kituo cha polisi kuhusiana na tukio hilo
Kwa upande wake Suma mnazareti ambae nae alikuwa member wa Mtanashati Entertainment amesema kuwa Ustadhi juma na musoma hajamtimua ila yeye mwenyewe ameondoka katika Crew hiyo na ameamua kuachana na kundi hilo coz ameona halina malengo ya kumfikisha mbali.
Suma mnazareti amesema ''ustadhi juma na musoma amekuwa akitoa hela nyingi kwa maprezenter wa hapa mjini na ma Dj ili wapige miziki ya Watanashati" na kuongeza kuwa eti yeye hawezi kuwa kama PNC au Dogo janja coz Pnc alimuokota huko gongo lamboto akiwa hana sehemu ya kulala ndio maana akampangishia chumba na Dogo janja anakaa kwa Ustadhi juma hivyo basi hata wakionewa hawawezi kuongea coz yeye ameshika maisha yao.
''Mimi ni mtu ambaye nimeshatoka nyumbani kwetu {nimepanga} na ninaishi na mtu kwa hiyo ninalipa chumba na mambo mengine hivyo basi ni bora nifanye hustle zangu coz ninataka nifanye mziki utaonitangaza mpaka nje ya nchi........!!
NB: Kwa mujibu wa Suma mnazareti ni kwamba ukiwa mtanashati ni lazima katika nyimbo yako umtaje {umrushe} ili aone kama nyimbo yako ndio nzuri vinginevyo hakuelewi na ndio mana kama ni msikilizaji mzuri wa mziki nyimbo zinazoimbwa na wanamuziki kutoka Mtanashati Ent. ni kweli kwamba lazima utalisikia jina la Ustadhi juma na musoma.!
No comments